Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya wahamiaji 1400 kutoka Libya wamezama kwenye bahari ya Mediteranian: UNHCR

Zaidi ya wahamiaji 1400 kutoka Libya wamezama kwenye bahari ya Mediteranian: UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR linasema kuwa zaidi ya wahamiaji 1400 wamezama kwenye bahari ya Mediteranian kwa muda wa miezi miwili iliyopita wanapojaribu kuikimbia Libya wakitumia mashua mbovu na zilizobeba kupita kiasi.

Kwenye kisa cha hivi majuzi watu 600 wanaaminika kuzama maji Ijumaa iliyopita baada ya mashua waliyokuwa wakitumia kupatwa na matatizo muda mfupi baada ya kuondoka mjini Tripoli. Hata hivyo UNHCR inasema kuwa idadi kamili ya waliokufa bado haijulikani. Mashirika ya kibinadamu yanatoa wito kwa jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi NATO na makampuni ya usafiri wa bahari kwenye bahari ya Mediteranian kusaidia katika kuwakoa wahamiaji wanaojaribu kuingia kweye visiwa vya Lampedusa na Malta wakitumia mashua zilizojaa kupita kiasi. Melisa Fleming ni kutoka UNHCR.

(SAUTI YA MELISA FLEMING)