Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN-HABITAT na Kuwait waendesha kongamano la usalama mijini

UN-HABITAT na Kuwait waendesha kongamano la usalama mijini

Wajumbe 52 kutoka duniani kote wamekuwa na mkutano huko Kuwait City kujadilia mipango itayoweka vipaumbele vya kuwepo kwa hali ya usalama kwenye maeneo ya mijini kwa ajili ya kukuza maendeleo endelevu.

Mkutano huo ambao umesimamiwa na Waziri wa kazi za umma na tawala za manispaa wa Kuwait Bwana Fadhel Safar,umewahusisha wataalamu wa majiji pamoja na maeneo mengine.

Washiriki hao wamajadilia njia zitazokaribisha mashirikiano zaidi ili hatimaye kufikia shabaya ya pamoja ya kuwa na maendeleo endelevu. Mkutano huo umefanyika kwa ushirikiano wa pamoja baina ya serikali ya Yemen na shirika la umoja wa mataifa linalohusika na makazi UN-HABITAT.