Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakunga wana jukumu muhimu katika jamii:UNFPA

Wakunga wana jukumu muhimu katika jamii:UNFPA

Kila siku maelfu ya wanawake duniani wanakufa wakati wa kujifungua, lakini vifo vingi vingeweza kuzuiwa kwa msaada ya wakunga waliopata mafunzo yanayostahili.

Mai 5 ni siku ya kimataifa ya wakunga na shirika la Umoja wa Mataifa la mfuko wa idadi ya watu UNFPA unaelezea jukumu muhimu walilonalo wakunga na kusema ni zaidi ya kuzalisha.

Anne Wittenberg kutoka UNFPA anasema kujifunguwa bila kuangaliwa ipasavyo kunaweza kuwa na hatari kubwa kwa maisha ya mamilioni ya wanawake.

(SAUTI YA ANNE WITTENBERG)

Amesema jukumu la wakunga ni kuwa zaidi ya kusaidia kuzalisha watoto na mwezi Juni mwaka huu UNFPA itatoa ripoti ya kwanza kabisa kuwahi kutolewa kuhusu hali ya huduma za ukunga.