Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu limepitisha azimio kulaani mauaji Syria

Baraza la haki za binadamu limepitisha azimio kulaani mauaji Syria

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa mataifa limepitisha azimio kulaani yanayoendelea Syria. Azimio hilo limepita kwa kura 26 za ndio, 9 za hapana na 7 hawakupiga kura kabisa.

Baraza limefahamishwa kuwa zaidi ya watu 420 wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa wakati wa maandamano ya kuipinga serikali nchini Syria.

Akilihutubia baraza hilo wakati wa kuanza kwa kikao cha kujadili hali nchini Syria naibu mkuu wa masuala ya haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Kyung-wah Kang amesema kuwa ripoti kutoka nchini Syria zinaonyesha ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu uliondeshwa na vikosi vya usalama.

Amesema kuwa jambo la kusikitisha ni kuwa serikali serikali ya Syria imeenda kinyume na matarajio yake ya kutekeleza mabadiliko ya kisiasa na ya kiuchumi na badala yake kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji wenye amani.

(SAUTI YA KYUNG-WAH KANG)