Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya watu Ivory Coast wako katika hali mbaya:OCHA

Maelfu ya watu Ivory Coast wako katika hali mbaya:OCHA

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema kuwa maelfu ya watu kusini na magharibi mwa Ivory Coast wanahitaji zaidi misaada ya kibinadamu.

Linasema kuwa hatua zaidi zinahitaji kuchukuliwa kuwalinda raia na waaathiriwa wa vitendo vya ubakaji na dhuluma zingine, vitendo vinavyoendelea kushuhudiwa katika maeneo ambayo bado si salama.

OCHA linasema kuwa hata baada ya jitihada za jamii ya kimataifa kuwasaidia wananchi na serikali ya Ivory Coast, bado ukosefu wa usalama unatatiza jitihada za kutoa misaada kwenye maeneo kadha ya mji wa Abidjan. Elizabeth Byrs kutoka OCHA anaeleza.

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)