Mtaalamu wa UM ashtushwa na mauaji ya Kerroumi Algeria

27 Aprili 2011

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya uhuru wa maoni na kujieleza Frank La Rue leo ameelezea kushtushwa kwake na huzuni kubwa kutokana na mauaji ya mwanaharakati wa kisiasa aliyekutana naye hivi karibuni alizozuru nchini Algeria.

La Rue alikutana na Ahmed Kerroumi ambaye alikuwa profesa kwenye chuo kikuu cha Oran na mwanachama wa chama cha upinzani cha Democratic and Social movement alipikuwa ziarani nchini humo Aprili 10 hadi 17 mwaka huu.

Baada ya kutoweka kwa siku kadhaa maiti ya profesa Keroumi ilikuwa ofisini mwake April 23. George Njogopa anaarifu.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter