China na IOM wazindua mradi kushughulikia wahamiaji

China na IOM wazindua mradi kushughulikia wahamiaji

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na wizara ya mambo ya kigeni nchi China wamezindua awamu ya pili ya mradi unaoshughulika na masuala ya uhamiaji mjini Beijing.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo mkurugenzi wa IOM William Lacy Swing amesema kuwa IOM itandelea kushirikiana na serikali ya China kukomesha usafirishaji haramu wa watu na pia kuhakikisha kuwepo kwa ajira kwa wahamiaji na katika kulinda haki za wahamiaji wafanyikazi.

Awamu ya kwanza ya kutoka mwaka 2007 hadi 2010 ilitoa mafunzo kwa maafisa 400 wa kichina ambao waliwafikia wahamiaji milioni 1.5 kupitia kwa kampeni za kuzuia uhamiaji. Awamu ya pili itahakikisha mafanikio kwa awamu ya kwanza. Mradi huo wa miaka mitatu unafadhiliwa na jumuiya ya Ulaya, Italia, IOM, ILO na Marekani.