Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IMF yaongeza muda wa mkopo kwa nchi ya Pakistan

IMF yaongeza muda wa mkopo kwa nchi ya Pakistan

Bodi kuu ya shirika la fedha duniani IMF juma hili imeidhinisha kuongezwa kwa muda wa miezi tisa wa kutoa mkopo kwa nchi ya Pakistan hadi mwezi Septemba mwaka 2011.

Kuongezwa kwa muda huo kutatoa fursa kwa serikali ya Pakistan kufanyia mabadiliko sekta zake zake ikwemo sekta ya ushuru pamoja na sekta za kifedha.

Wafanyikazi wa IMF wataendelea na mazungumzo na serikali ya Pakistan kuhusu mpango huo. Awali IMF iliidhinisha mkopo wa dola bilioni 7.61 mwezi Novemba mwaka 2008 na kuongezwa hadi mwezi Disemba mwaka huu ukiwa mkopo wa dola bilioni 10.