Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wajikuta ndani ya mzozo Yemen:UNICEF

Watoto wajikuta ndani ya mzozo Yemen:UNICEF

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa watoto nchini Yemen wanaendelea kuathirika na mzozo wa kisiasa unaoendelea kushuhudiwa nchini humo.

Kati ya mwezi wa Februari na Aprili mwaka huu watu 26 wameuawa na wengine 36 kujeruhiwa kwa njia ya risasi huku wengine 47 wakifa kwa kupigwa .

Watoto wengine 763 wamekabiliana na gesi za kutoa machozi. Kwa sasa UNICEF inatoa wito kwa pande husika nchini Yemen kuwalinda watoto kutoka na mambo kama haya.