Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM yaongeza kasi ya kugawa misaada Libya

Mashirika ya UM yaongeza kasi ya kugawa misaada Libya

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linatuma meli iliyosheheni msaada kuelekea mjini Misrata nchini Libya msaada ambao unaweza kuwasaidia kati ya watu 15,000 na 20,000.

Kwenye msaada huo kuna vifaa vya kutoa huduma za kwanza na vifaa vya watoto vya kuchezea. UNICEF inasema kuwa hali katika mji wa Misrata inazidi kuwa mbaya huku watoto wakiathirika zaidi na kuongeza kuwa imethibitisha vifo ishirini vya watoto kwenye mji huo.

UNHCR pia inasema kuwa imeshuhudia idadi kubwa ya wakimbizi wanaowasili nchini Tunisia kutoka magharibi mwa Libya. Inakadiria kuwa walibya 10,000 wamevuka mpaka na kuingia Tunisia kwa muda wa siku 10 zilizopita. Andrej Mahecic ni kutoka UNHCR.

(SAUTI YA ANDREJ MAHECIC)