Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa ajira umechangia machafuko Afrika Kaskazini:ILO

Ukosefu wa ajira umechangia machafuko Afrika Kaskazini:ILO

Shirika la kazi duniani ILO linasema mashafuko yanayoendelea Afrika ya Kaskazini na Mashariki ya Kati ni matokeo ya kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira hususan kwa vijana.

Shirika hilo linasema kutokuwepo na demokrasia ya kweli pia kumechangia na mambo yote haya yanapaswa kushughulikiwa ili kuzuia jamii kusambaratika katika eneo hilo.

ILO inasema serikali zinahitaji kushirikiana na mashirika ya kazi na jumuiya za wafanyakazi hasa katika kuunda nafasi za ajira na mipango ya kuilinda jamii katika masuala ya kazi.