Skip to main content

Kilimo cha kasumba kupungua Afghanistan 2011:UNODC

Kilimo cha kasumba kupungua Afghanistan 2011:UNODC

Kilimo cha kasumbu kinatarajiwa kupungua kwa mwaka huu wa 2011 nchini Afghanistan licha ya bei ya juu ya zao hilo imesema ripoti ya utafiti iliyotolewa leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC.

Kwa mujibu wa UNODC kupungua huko kutasababishwa na kiwango kidogo cha uzalishaji kwenye mikoa ya Himand na Kandahar. Hata hivyo ripoti hiyo imesema kwenye maeneo kama Badakshan, Baghlan na Faryab majimbo ya Kaskazini na Kaskazini mashariki kilimo cha kasumba kitaongezeka .

Kilimo cha kasumbu kwenye mikoa ya Hilmand na Kandahar kimekuwa kikipungua kwa karibu miaka miatatu sasa kutoka ekari 103,590 mwaka 2008 hadi ekari 65,045 mwaka 2010. Pia ari ya kisiasa ya serikali kukabiliana na kilimo hicho imechangia kupungua kwa uzalishaji.