Deiss aeleza umuhimu wa ushirikiano kwenye baraza kuu la UM

Deiss aeleza umuhimu wa ushirikiano kwenye baraza kuu la UM

Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa amewashauri wanachama wa baraza hilo kulifanya kuwa baraza lililo na nguvu katika kutoa huduma zake duniani .

Joseph Deiss amesema kuwa ili baraza kuu lipate kutekeleza wajibu wake katika uongozi hususan kwa kujenga ushirikiano na pande zingine zilizo na ushawishi duniani kama vile nchi tajiri na zile zinazoinukia kiuchumi duniani za G-20.

Bwana Deiss pia ameelezea umuhimu wa kuwepo ushirikiano kati ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa na mashirika mengine makuu ya Umoja wa Mataifa kama moja ya njia ya kuleta mshikamano. Tangu ashike wadhifa wa urais Deiss amefanya mikutano kadha na wakuu mbali mbali wa mabaraza likiwemo baraza la usalama, baraza la uchumi na haki za binadamu na tume ya amani.