Skip to main content

UM wahofia hali ya wafanyakazi wahamiaji Libya

UM wahofia hali ya wafanyakazi wahamiaji Libya

Kamati ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na haki za wahamiaji wameelezea hofu kubwa waliyonayo kuhusu kunyanyaswa kwa wafanyakazi wahamiaji na familia zao nchini Libya na hasa wahamiaji kutoka nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara.

Kamati hiyo ya kulinda haki za wahamiaji wote na familia zao pia imeelezea hatari ya madhara kwa wahamiaji hao baharini na mipakani.

Imesema imeshitushwa sana na tukio la karibuni la kuzama kwa zaidi ya wahamiaji 200 kwenye pwani ya Italia ambapo miongoni mwa wengi waliopoteza maisha ni wanawake na watoto waliokuwa wakijaribu kukimbia machafuko Libya. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)