Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katika mkutano wa kimataifa kuhusu Libya UM wasisitiza kipaumbele ni kuwalinda raia

Katika mkutano wa kimataifa kuhusu Libya UM wasisitiza kipaumbele ni kuwalinda raia

Mkutano maalumu wa kujadili hali ya Libya umeanza hii leo mjini Doha Qatar ukihudhuriwa na pande mbalimbali.

Mkutano huo unajumuisha wadau mbalimbali wakiwemo NATO, Jumuiya ya nchi za Kiarabu, Muungano wa Afrika, waasi wanaompinga Rais Muammar Qhadafi ambao wanashiriki kwa mara ya kwanza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Mkutano huo umetokana na tume maalumu iliyoundwa kuhusika moja kwa moja na suala la Libya baada ya mkutano wa mawaziri uliofanyika Machi 29 mjini London ukihudhuriwa na wajumbe kutoka Ulaya, Marekani, Mashariki ya Kati na mashirika kadhaa ya kimataifa.

Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema lengo la jumuiya ya kimataifa liko bayana nchini Libya nalo ni kuhakikisha raia wanalindwa na ameonya juu ya hali ya kibinadamu kuzidi kuwa mbaya kutokana na machafuko yanayoendelea na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuwa na msimamo mmoja na kauli moja.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Masuala muhimu yanayojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na kuwapa msaada wa kisiasa , kijeshi na kifedha waasi hao wanaompinga Qadhafi na pia kutolewa ufafanuzi wa mchango wa NATO katika hali nzima inayoendelea.