Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa UM asikitishwa na Marekani iliyomzuia kumuona askari gerezani

Mtaalamu wa UM asikitishwa na Marekani iliyomzuia kumuona askari gerezani

Mtaalamu wa kujitegemea anayefanya kazi na umoja wa mataifa katika masuala ya mateso Juan Mendez amesema kuwa amesikitishwa na kuvunjwa moyo baada ya kushindwa kuonana na askari mmoja anashikiliwa na serikali ya Marekani.

Askari huyo Bradley Manning alikamatwa May mwaka jana nchini Iraq akituhumiwa kuwa alisaidia kutoa taarifa nyeti kwa mtandao wa WikiLeaks.

Mtaalamu huyo wa masuala ya mateso ameeleza kuwa licha ya jitihada zake kuomba ruksa ya kwenda kuonana na askari huyo katika mazingira huru na binafsi lakini serikali ya Marekani imeendelea kutia ngumu.

Amesema kuwa anatiwa wasiwasi na afya ya askari huyo ambaye amezuiliwa kwenye gereza la kijeshi huko Virginia.