Skip to main content

UM wataja majina ya waliokufa kwenye ajali ya ndege DRC

UM wataja majina ya waliokufa kwenye ajali ya ndege DRC

Ofisi ya umoja wa mataifa imetangaza majina ya watu waliopoteza maisha kwenye ajali ya ndege iliyotokea huko Jamhuri ya Congo jumatatu na kuuwa watu wote 33 akiwemo rubani wa ndege hiyo kutoka umoja wa mataifa.

Ndege hiyo iliyokuwa ikiruka kutoka eneo la Kaskazini mashariki wa mji wa Kisangani ilianguka na kuvunjika vipande vipande wakati ikijaribu kutua kwenye mjini Kinshansa kufuatia hali ya mvua kubwa na mawingu iliyotanda kwenye eneo hilo.

Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa wamefanikiwa kutambua miili ya marehemu hao na kinachofanyika sasa ni kuwatambua ndugu wa karibu. Uchunguzi juu ya ajali hiyo tayari umeanzishwa.