Skip to main content

Makao makuu ya UNOCI yashambuliwa Ivory Coast

Makao makuu ya UNOCI yashambuliwa Ivory Coast

Makao makuu ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini Cote D\' Ivoire UNOCI yameshambuliwa jana jioni na majeshi ya Laurent Gbagbo yaliokuwa yamepiga kambi katika wizara ya ulinzi, si mbali sana na ikulu.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa vilijibiza mashambulio hayo karibu muda wa saa tatu. Wakati huo huo , Majeshi ya Umoja wa Mataifa yanayofanya doria kuimarisha usalama katika uwanja wa ndege wa Abidjan, unaodhibitiwa na vikosi hivyo vya UNOCI, pia walishambuliwa na makundi ya vijana.

Hatimae saa moja usiku, vikosi vya Umoja wa Mataifa vilishambuliwa karibu na kituo cha Redio na Televisheni ya Taifa ( RTI)