Nchi za Caribbean hazijajiandaa vyema na janga la tsunami:UM

28 Machi 2011

Umoja wa Mataifa umesema kuwa jaribio la kwanza la kubaini ubora wa maandalizi ya athari za kutokea kwa tsumani kwenye eneo la Caribbean umebainisha kuwa kuna haja ya kuimarisha maandalizi zaidi ikiwemo mawasiliano na mipango ya uokoaji .

Jaribio hilo lililofahamika kama Caribe Wave 2011 liliendeshwa mnamo tarehe 23 mwezi huu na kuzijumuisha nchi 34. Kwenye jaribio hilo kulibuniwa tetemeko la ukubwa wa 7.6 kwenye vipimo vya richter pwani mwa visiwa vya Virgin na kusababisha kutokea kwa mawimbi yenye urefu wa mita kumi.

Jaribio hilo lilionyesha matatizo yaliyopo katika mawasilino baada ya baadhi ya maeneo kukosa kupokea onyo la jaribio hilo. Mkurugenzi wa shirika la elimu , sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Irina Bokova amesema kuwa majaribio kama hayo ni muhimu katika kuhakikisha kuwa kuna maandalizi ya kutosha kunapotokea janga.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter