Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano wa buniwa kupunguza uchafuzi wa bahari:UNEP

Ushirikiano wa buniwa kupunguza uchafuzi wa bahari:UNEP

Waakilishi wa serikali , viwanda vikubwa na watafiti wa mambo ya bahari wameungana kutafuta mbinu mpya za kukabiliana na tatizo la kuendelea kuchafuliwa kwa bahari kuu duniani.

Hata baada ya muda mrefu wa jitihada za kupunguza uchafu baharini kama vile bidhaa za plastiki , nyavu za uvuvi zilizoachwa na takakata ya viwandani bado tatizo hili linaendelea kukithiri.

Baada kuletea pamoja wataalamu kutoka nchi 35, mashirika ya utafiti na makampuni makubwa kwenye mkutano wa tano wa kimataifa kuhusu kuchafuka kwa bahari, kuliafikiwa makubaliano ya kutatua tatizo la kuchafuka kwa bahari katika ngazi za kimataifa na kitaifa.

Mkutano huo ulioandaliwa na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na kufanyika mjini Honolulu Hawaii kuanzia tarehe 20 hadi 25 mwezi huu ni kama mwanzo mpya katika jitihada za kupunguza kuchafuka kwa bahari, athari katika uchumi na afya kwa binadamu.