Baada ya duru ya pili ya uchaguzi Haiti yasubiri matokeo

21 Machi 2011

Hamasa inaongezeka nchini Haiti wakati mamilioni ya watu wakisubiri matokeo ya uchaguzi wa Rais wa duru ya pili uliofanyika jana Jumapili.

Mke wa zamani wa Rais Bi Mirlande Manigat na mwanamuziki nyota Michel Martelly wameingia katika kinyang'anyiro hicho cha duru ya pili ambacho kilicheleweshwa mwa miezi miwili. Duru ya pili ya uchaguzi ilicheleweshwa wakati yalipozuka machafuko baada ya matokeo ya duru ya kwanza hapo Desemba mwaka jana.

Mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti MINUSTAH umewataka Wahaiti kuwa wavumilivu na kujizuia kufanya vitendo vya ghasia wakati wakisubiri matokeo ambayo yanatarajiwa kuchukua siku kadhaa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter