Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubaguzi wa rangi dhidi ya wenye asili ya Afrika unaendelea:UM

Ubaguzi wa rangi dhidi ya wenye asili ya Afrika unaendelea:UM

Kila mwaka dunia inaadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya Sharpeville ya mwaka 1960 ambapo mamia ya waandamanaji waliuawa baada ya kupigwa risasi na polisi walipokuwa wakipinga sheria za ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini.

Leo ukiwa ni mwaka wa 41 kuadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza ubaguzi wa rangi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mwaka huu umetengwa katika kukabili ubaguzi unaowakumba watu wenye asili ya Afrika na hatua hiyo inakwenda sambamba na azimio la baraza kuu la Umoja wa Mataifa ambalo limeufanya mwaka huu wa 2011 kuwa ni mwaka wa watu wenye asili ya Afrika.

Ban amesema ubaguzi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika unasikitisha na unawafanya mara nyingi kukwama kwenye umasikini, wanakosa elimu kwa sababu ya ubaguzi jambo linalowafanya kutopata kazi za maana.

Amesema hii si haki ni makosa ya kihistoria yakijumuisha pia biashara ya utumwa ambayo athari zake bado zipo mpaka leo. Waafrika wenyewe wana maoni gani kuhusu siku hii.

(MAONI YA UBAGUZI WA RANGI)