Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makubaliano ya Brazili na Marekani yaifurahisha ILO

Makubaliano ya Brazili na Marekani yaifurahisha ILO

Mkurugenzi wa shirika la kazi duniani ILO Juan Somavia ameyakaribisha maelewano yaliyo tiwa sahihi kati ya serikali ya Marekani na Brazil yaliyo na lengo la kutatua tatizo la ukosefu wa ajira na masuala mengine ya kijamii kati ya mataifa hayo.

Maelewano hayo yalitiwa sahihi na balozi wa Marekani nchini Brazil Thomas Shannon na waziri wa masuala ya kigeni wa Brazil Antonio Patriota wakati wa ziara ya rais wa Marekani Barack Obama nchini Brazil.

Kati ya yanaohitajika kutekelezwa kwenye makubalino hayo ni kuwepo kwa ajira bora na za kisasa , haki ya kufanya kazi , usawa katika kazi pamoja na manuafaa mengine kama ile ya kiafya.