Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM kuchunguza visa vya watu kutoweka

Wataalamu wa UM kuchunguza visa vya watu kutoweka

Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa linalohusika na watu kutoweka limetathimini visa 11 ambavyo vinahitaji kuchukuliwa hatua za haraka nchini Mexico.

Wataalamu hao waliokuwa Mexico City kuanzia Machi 15 hadi 18 pia wamepitia taarifa ya visa 190 vya kesi zilizowasilishwa za watu kutoweka katika nchi mbalimbali. Watu hao wametoweka nchini Bangladesh, Uchina, Colombia, Congo Brazzaville, Korea, Misri, Georgia, India, Iraq na Lebanon.

Nchi zingine ni Mexico, Morocco, Pakistan, Hispania, Sri Lanka, Syria, Thailand, Tunisia, Turkmenistan, Uzbekistan, Venezuela na Yemen. George Njogopa anaarifu.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)