Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaorodhesha madawa 30 kunusuru maisha ya mama na mtoto

WHO yaorodhesha madawa 30 kunusuru maisha ya mama na mtoto

Shirika la afya duniani WHO leo limetoa orodha ya kwanza kabisa ya madawa yanayopewa kipaumbele kwa afya ya mama na mtoto ambayo yanahitaji kupatikana kila mahali ili kuokoa maisha ya watu hao.

WHO inasema madawa muafaka ni muhimu katika kufikia malengo ya kimataifa ya afya, kwani watoto zaidi ya milioni nane wenye umri wa chini ya miaka mitano bado wanakufa kila siku kwa magonjwa kama kichomi, kuhara na malaria, huku wanawake takribani 1000 wanakufa kila siku kutokana na matatizo wakati wa ujauzito na kujifungua.

Shirika hilo linasema vifo vyote hivyo vinatokea katika nchi zinazoendelea na vingi vingeweza kuepukwa endapo madawa muafaka yangepatikana. Sasa inasema orodha hiyo ya madawa 30 itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo hivyo.