Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa masuala ya lishe wa WHO wakabiliana na utapiamlo

Wataalamu wa masuala ya lishe wa WHO wakabiliana na utapiamlo

Shirika la afya duniani WHO pamoja na wataalamu wengine wa kimataifa wametoa wito wa kuchukuliwa hatua mpya za kumaliza utapiamlo na matatizo mengine ya kifya yanayowaathiri mamilioni ya watu duniani.

Mkurugenzi wa masuala ya lishe kwa maendeleo ya kiafya kwenye shirika la WHO Dr Francesco Branca anasema kuwa utapiamlo unachangia asilimia 11 ya maradhi na afya duni.

Alice Kariuki na taarifa kamili

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)

WHO inatoa uongozi wa kimataifa kuhusu viwango viwango vya lishe . WHO pia imeombwa kutoa ushauri na kuchukua hatua zinazohitajika ili kuzisadia nchi na watu husuasan watoto wachanga na wanawawake.

Ripoti zinasema kuwa watoto milioni 13 wanaozaliwa kila mwaka wana uzito wa chini ikimaanisha kuwa hawakukua kwa njia inayofaa wakiwa bado tumboni mwa mama zao. Kuanzia tarehe 14 hadi 18 mwezi huu kundi la wataaalmu la kutoa ushauri la WHO llinalokutana mjini Geneva liatakuwa na jukumu la kutoa ushauri kuhusu utapiamlo. Kundi hilo linatarajiwa kutoa mapendekezo kuhusu njia za kukabiliana na ugonjwa wa anaemia. Inakadiriwa kuwa kwenye nchi zinazoendelea karibu asilimia 40 ya watoto wanaokwenda shuleni wana ugonjwa wa anaemia ambao huchangia asilimia 20 ya vifo vya watoto.