Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya kibinadamu Sudan kusini na Abyei hairidhishi - Chande

Hali ya kibinadamu Sudan kusini na Abyei hairidhishi - Chande

Mtaalamu binafsi wa masuala ya hali ya haki za binadamu nchini Sudan jaji Mohamed Chande Othman kutoka Tanzania amehitimisha ziara yake ya tathimini ya hali ya haki za binadamu Sudan Kusini.

Jaji Othman aliyekuwa Sudan Kusini kwa ziara ya siku nane amezuru pia jimbo la Darfur, kutembelea kambi za wakimbizi wa ndani ikiwemo ya Zamzam na kukutana na viongozi wa Kusini na Kaskazini. Amesema mapigano katika jimbo la Abyei yanazidi kuwafungisha virago raia, mfumo wa sheria hautendi haki na huduma za kibinadamu ni duni.

(SAUTI YA JAJI CHANDE OTHMAN)

Jaji Othman pia ametoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini na Kaskazini kushirikiana kwa karibu na jumuiya ya kimataifa ili kuhakikisha watu wanalinda, haki za binadamu hazikiukwi na mfumo wa sheria unafuatwa. Kwa mujibu wa shirika la OCHA watu 20,000 wamelikimbia jimbo la Abyei hasa eneo la Jonglei na kambi ya wakimbizi wa ndani ya Zamzam imeshuhudia wimbi jipya wa wakimbizi 53,000.