Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali imeanza kuwa shwari mjini Tripoli Libya:UM

Hali imeanza kuwa shwari mjini Tripoli Libya:UM

Mwakilishi mpya wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuratibu masuala ya kibinadamu nchini Libya amewasili mjini Tripol.

Bwana Rashid Khalikov anaanza maandalizi ya mpango wa kutathimini masuala ya kibindamu nchini humo ambako amesema ameshuhudia hali ya utulivu iliyoanza kurejea katika mji mkuu Tripol, amesema maduka mengi yako wazi na watu wanatembea kwa uhuru bila bugudha mjini humo.

Hata hivyo mwakilishi huyo na timu yake wamesema wameshuhudia misururu mirefu ya wafanyakazi wahamiaji kwenye uwanja wa ndege wa Tripol na kwenye makambi ya muda yaliyoko nje ya uwanja wa ndege, huku kukiwa na mlolongo wa malori yanayowasafirisha wahamaiaji na hususan wa Kiafrika kuelekea kwenye mpaka baina ya Libya na Tunisia ambako watasafirishwa kurejea makwao.

Hadi sasa watu zaidi ya 267, 000 wamekimbia machafuko Libya, huduma muhimu kama chakula , malazi na madawa zinahitajika na fedha zilizoombwa kushughulikia matatizo ya Libya ni asilimia 47.7 tuu ndio zilizopatikana.