Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suluhu ya kumalizika serikali ya mpito ya Somalia ni muhimu:MAHIGA

Suluhu ya kumalizika serikali ya mpito ya Somalia ni muhimu:MAHIGA

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Augustine Mahiga amekuwa na mkutano na viongozi wa serikali ya mpito mjini Moghadishu mwishoni mwa wiki.

Mwakilishi huyo Balozi Augustine Mahiga na Rais wa Somalia Sheikh Sharif Ahmed na waziri wa mambo ya nje wa Somalia Mohammad Abdullahi Omar wamejadili kuhusu kumalizika kwa kipindi cha mpito , usalama na mapigano ya hivi karibuni kati ya majeshi ya serikali na wanamgambo yaliyosababisha vifo vya raia, na pia wanajeshi wa serikali na wa muungano wa Afrika AMISOM. Mahiga amesema kikubwa ni jinsi gani serikali itakavyosaidia kurejesha amani na kumaliza kipindi cha mpito bila purukshani.

(SAUTI YA AUGUSTINE MAHIGA)