Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya tetemeko na tsunami sasa mionzi ya nyuklia yatia hofu Japan:IAEA

Baada ya tetemeko na tsunami sasa mionzi ya nyuklia yatia hofu Japan:IAEA

Shirika la nyuklia na usalama wa viwanda Japan NISA limeliarishu shirika la kimataifa la nguvu za atomc IAEA kuhusu mlipuko uliotokea leo kwenye mtambo wa tatu wa kinu chache cha nyuklia cha Fukushima Daiichi.

Mlipuko wa gesi ya haydrogen umetokea leo Machi 14 majira ya asubuhi saana za Japan. Kwa mujibu wa NISA wafanykazi wote wako salama na hakuna aliyearifiwa kufariki dunia, ingawa watu sita wamejeruhiwa.

Ofisi ya kitengo hicho bado inaendelea kufanya kazi na shirika la IAEA linaendelea kuwasiliana kwa karibu na serikali ya Japan na kuangalia hali nzima na athari zake. Hofu imeanza kujitokeza kuhusu mionzi ya nyuklia na serikali imewataka watu wanaoshi maeneo ya karibu na mtambo huo kutotoka nje.