Skip to main content

Idadi ya waliokufa Japan inaongezeka na msaada unahitajika:OCHA

Idadi ya waliokufa Japan inaongezeka na msaada unahitajika:OCHA

Shughuli za kutafuta maelfu ya watu ambao hadi sasa hawajulikani waliko kufuatia tetemeko na tsunami nchini Japan zinaendelea. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA zaidi ya watu 2800 wamefariki dunia na maelfu hawajapatikana.

Timu 15 za wataalamu wa kimataifaifa zimepelekwa Japan ili kuisaidia serikali kukabiliana na mitetemo mingine inayoendelea kutibua tsunami kwenye ukanda wa Pacific. Hali ya tahadhari inaendelea nchini humo hasa sasa ambao hofu ya kusambaa mionzi ya nyuklia imetanda. Elizabeth Byrs ni msemaji wa OCHA.

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)

Hadi sasa watu 380,000 wamehamishwa kutoka maeneo yaliyoathirika na tetemeko na tsunami na kuhifadhiwa kwenye vituo vya dharura 2050. Watu wanakabiliwa na upungufu wa bidhaa muhimu kama chakula, maji na maeneo mengi hayana nishati ya umeme.