Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano wa kimataifa utapunguza adha za kiuchumi:UM

Ushirikiano wa kimataifa utapunguza adha za kiuchumi:UM

Baada ya ulimwengu kushuhudia hali ngumu ya kiuchumi iliyosababisha kukwama kwa miradi mingi ya kimaendeleo na wakati pia ulimengu ukiendelea kukumbwa na kupanda kwa gharama ya chakula na nishati kunahitajika kuchukuliwa hatua zitakazochangia zaidi katika maendeleo.

Haya ni kwa mujibu wa mkuu wa baraza la uchumi na masuala ya jamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC Lazarous Kapambe ambaye amesema kuwa kuwepo ushirikiano wa nchi zote kunaweza kuleta maendeleo na pia kuchangia kutimizwa kwa malengo ya milenia.

Bwana Kapambwe ameongeza kuwa jamii ya kimataifa kwa sasa inakabiliwa na changamoto kwenye maafikiano ya kutimizwa kwa malengo ya milenia ifikapo mwaka 2015.