Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei za chakula hazijabadilika sana mwezi Machi:FAO

Bei za chakula hazijabadilika sana mwezi Machi:FAO

Bei za chakula kwa mwezi wa Machi hazina tofauti na zile za mwezi wa Februari kwa mujibu wa ripoti za bei ya chakula za shirika la chakula na kilimo FAO zilizotolewa Alhamisi.

Ripoti hizo zinasema kwa wastani kumekuwa na pointi 216 mwezi wa Machi ikilinganishwa na pointi 215 za Februari.

Katika vyakula mbalimbali hali haijabadilika isipokuwa bei ya mafuta tuu ndio iliyoimarika huku ya bidhaa za maziwa ikishuka.

Bei ya nafaka kama mahidi imeimarika kidogo, na soko la mbaazi, wakati bei ya ngano imesalia bila mabadiliko.

Uchina na Nigeria zimetajwa kuwa ni wanunuzi wakubwa wa chakula kwa mwezi wa Machi.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)