Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Israel isitishe bomoabomoa ukingo wa Magharibi:UM

Israel isitishe bomoabomoa ukingo wa Magharibi:UM

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa Richard Falk ametoa wito kwa uongozi wa Israel kusitisha mara moja bomoabomoa ya nyumba za Wapalestina inayoifanya kinyume cha sheria kwenye Ukingo wa Magharibi.

Amesema bomoabomoa hiyo itazilazimisha familia 15 ambazo ni jumla ya Wapalestina 150, wakiwemo watoto kukosa makazi kwenye eneo la Beit Hanina Mashariki mwa Jerusalem.

Amesema hatua ya kuwahamisha kwa nguvu, kubomoa nyumba zao, upanuzi wa makazi ya walowezi na matumizi ya nguvu dhidi ya Wapalestina kwenye eneo linalokaliwa la Jerusalemu Mashariki ni ukiukaji wa haki za binadamu na mkataba wa Geneva. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)