Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada zaidi unahitajika kwa Ivory Coast:UM

Msaada zaidi unahitajika kwa Ivory Coast:UM

Mashirika ya misaada ya kimataifa yametoa wito wa msaada zaidi ili kukabiliana na matatizo ya kibindamu yanayoikumba Ivory Coast hivi sasa.

Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wanasema zahma ya Ivory Coast imewekwa kando wakati dunia ikijikita katika matukio yanayoendelea Afrika ya Kaskazini. UNHCR inasema idadi ya wakimbizi wa ndani inakaribia nusu milioni. 

Na UNICEF imeongeza kuwa upungufu wa madawa unakuwa kikwazo cha juhudi za kukabilinana na mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu, surua na homa ya manjano. Marixie Mecado kutoka UNICEF anasema watoto hawaendi tena shule kutokana na matatizo ya usalama.

(SAUTI YA MARIXIE MECADO)

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP kwa upande wake linasema kuwafikia wakimbizi na wakimbizi wa ndani Ivory Coast kuwapa msaada wa chakula inazidi kuwa vigumu kutokana na ukosefu wa usalama na mapigano. Kwa mujibu wa shirika hilo wakimbizi wa ndani zaidi ya 300,000 watapatiwa msaada wa chakula.