Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pande zinazozozana Sahara Magharibi zashindwa kufikia suluhu

Pande zinazozozana Sahara Magharibi zashindwa kufikia suluhu

Pande zinazozozana kuhusiana na eneo la Sahara Magharibi, zimeshindwa kuafikiana namna ya kutanzua mzozo huo wakati wajumbe wake walipokutana kwa majadiliano maalumu chini ya uratibu wa umoja wa mataifa.

Pande hizo Morocco na upande wa  Frente Polisario, ambao kila mmoja unang'ang'ania kumiliki eneo hilo, walionyesha tofauti zao pale kila upande uliposhindwa kuafikia mapendezo yaliyoletwa ambayo yangefungua ukurasa wa kuanzishwa majadiliano ya kusaka suluhu

 

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayefuatilia mzozo huo Christopher Ross amesema kuwa licha ya jitihada za kuwakutanisha wajumbe hao ili kuweka dira ya pamoja ya namna ya uendeshwaji wa majadiliano ya usakaji suluhu, lakini pande hizo zimeendelea na misimamo yao ya kukataa wazo hilo.

Mkutano huo ambao umefanyika nchini Malta umehudhiriwa na wajumbe kutoka nchi jirani za Algeria na Mauritania. Mkutano mwingine wa majadiliano unategemewa kufanyika tena mwezi May mwaka huu huku wajumbe wa pande zote wakichukua fursa ya kufuatilia zaidi pendekezo hilo