Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wa Afrika wanasafirishwa leo toka Libya:IOM

Wahamiaji wa Afrika wanasafirishwa leo toka Libya:IOM

Wakati shirika la kimataifa la uhamiaji IOM likiendelea kuwasafirisha maelfu ya wahamiaji wanaokimbia machafuko Libya kundi kubwa la Waafrika kutoka Kusini mwa jangwa la Sahara wanafanikiwa kutoroka kutoka Libya na kufika mipakani kupata msaada wa IOM.

Leo Machi 10 IOM inawasafirisha maelfu ya wahamiaji kutoka Bangladesh, Afrika, Ufilipino, Tunisia, Misri na Malta. Wengi wao wanarejea nyumbani na kundi kubwa la leo ni waafrika kutoka Nigeria, Ghana, Mali, Mauritania, Guinea, Niger, Togo, Sierra Leone na Cameroon.

Afisa habari na uhusiano wa IOM Jumbe Omari Jumbe aliyeko kwenye mpaka baina ya Libya na Tunisia anafafanua kuhusu idadi yao wahamiaji wanaorudishwa leo.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)