Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia lazima walindwe kwenye machafuko Libya:OCHA

Raia lazima walindwe kwenye machafuko Libya:OCHA

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Valerie Amos ametoa wito kwa pande zote husika kwenye mgogoro wa Libya kuwalinda raia.

Wito huo unafuatia taarifa kwamba kumekuwa na mapigano mazito na mashambulizi ya mabomu Magharibi mwa Libya, mapigano yaliyosababisha idadi kubwa isiyojulikana ya vifo na majeruhi. Bi Amos amesema pande zote katika mapigano lazima zichukue hatua kuhakikisha kwamba raia hawadhuriki.

Kwa kutambua umuhimu wa kuwalinda raia na kupata suluhu ya machafuko ya Libya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua mratibu mpya kuangalia masuala ya kibinadamu Libya bwana Rashid Khalikov ambaye amewasili katika eneo hilo na kuzungumza na waandishi wa wa habari

(SAUTI YA RASHID LHALIKOV)