Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zaidi zimetia sahihi mkataba kulinda bayo-anuai

Nchi zaidi zimetia sahihi mkataba kulinda bayo-anuai

Colombia, Denmark, Netherlands na Sweden zimekuwa nchi za kwanza kutia sahihi mkataba mpya kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ulio na sheria za kimataifa kuhusu hatua zitakazochukuliwa iwapo kutaokea uharibifu kwenye balojia anuai na viumbe unaosababishwa na viumbe vilivyofanyiwa mabadiliko ya kimaumbile.

Mkataba huo ulipitishwa mnamo tarehe 15 mwezi Oktoba mwaka uliopita mjini Nagoya Japan baada ya miaka kadha ya majadiliano. Mkataba huo unaofahamika kama Cartagena una lengo la kulinda baolojia kutokana na hatari inayotokana na viumbe vinavyoishi vilivyofanyiwa mabadiliko kutokana na teknolojia ya kisasa.

Hidenori Murakami ambaye ni mshauri wa waziri wa kilimo nchini Japan anasema kuwa mkataba huu utakuwa kama kinga dhihi ya uharibifu wote utakaosababisha na viumbe hivyo.