Wataalamu waliokuwa wanachunguza mafua ya H1N1 watoa ripoti:WHO

4 Machi 2011

Timu ya wataalamu wa kimataifa ambao wamekuwa wakichunguza hatua za kimataifa za kukabiliana na homa ya mafua ya H1N1 wameandaa ripoti.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO ripoti hiyo inayojumuisha masuala mbalimbali kuhusu hatua zilizochukuliwa na jinsi nchi zilivyokabili mafua ya ndege ya H1N1 hivi sasa imepelekwa kwa nchi wanachama ili kuweza kupata maoni yao.

Timu hiyo ya wataalamu itakutana mjini Geneva na nchi wanachama Machi 28 ili kukamilisha ripoti hiyo baada ya kupata maoni kutoka nchi mbalimbali.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter