Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM inaendelea kusafirisha wahamiaji waliokwama Libya

IOM inaendelea kusafirisha wahamiaji waliokwama Libya

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linaendelea kuwahamiasha maelfu ya wahamiaji waliokwama nchini Libya.

Jana Alhamisi wahamiaji 640 walisafirishwa kutoka mjini Benghazi na wahamiaji haoani raia kutoka Bangladesh ambao walisafirishwa kwa magari hadi kwenye mpaka wa Misri ambako IOM inawapa msaada wa chakula, huduma za afya na maji.

Wahamiaji wengine 300 wamesafirishwa leo wakiwemo 40 kutoka Afrika ya Magharibi ambao wanasemekana kuwa katika hatari kubwa zaidi kutokana na hali ya kuwalenga wahamiaji kutoka nchi za Afrika zilizoko Kusini mwa jangwa la Sahara.

Jumbe Omari Jumbe afisa uhusiano wa habari na mawasiliano wa IOM anafafanua kuhusu hali anayoishuhudia kwenye mpaka wa Tunisia na Libya kwenye uwanja wa ndege wa Jarba upande wa Tunisia wanakosafirishwa wahamiaji hao.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)