Serikali ya Somalia lazima ing'atuke na bunge kutekeleza mkataba wa Djibouti

3 Machi 2011

Serikali ya mpito ya Somalia na bunge la nchi hiyo lililojiongezea muda wa miaka mitatu wametakiwa kutekeleza makubalino ya amani ya Djibouti.

Hayo yamesisitizwa kwenye mkutano maalumu uliomalizika leo mjini Acca Ghana na kujumuisha bunge la Afrika, Umoja wa Mataifa na bunge la serikali ya mpito ya Somalia. Ajenda kubwa ni kulisaidia bunge la Somalia kuweza kutimiza wajibu wake katika kipindi hiki cha mpito.

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga aliyehudhuria mkutano huo amezungumza na Flora Nducha kuhusu mkutano huo.

(MAHOJIANO NA  AUGUSTINE MAHIGA)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter