Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano kuhusu hali ya ukame na mapigano Somalia

Mahojiano kuhusu hali ya ukame na mapigano Somalia

Somalia imeelezewa kuwa katika hatihati ya kutumbukia katika janga la kibinadamu endapo hatua muafaka za kuwasaidia mamilioni ya watu hazitochukuliwa.

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa aliyezuru nchi hiyo hivi karibuni Samshul Bari amesema hali ya ukame na machafuko ya vita baiana ya vikosi vya serikali ya mpito na kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab ynawaweka wakimbizi wa ndani na raia wa nchi hiyo katika njia panda.

Kuna tatizo kubwa la maji ya kunywa, upungufu wa chakula na pia madawa kutokana na athari za ukame zilizokwisha katili maisha ya watu, mifugo na kukausha baadhi ya vyanzo vya maji. Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii kuhusu hali halisi.

(MAHOJIANO NA BALOZI MAHIGA)