Mahojiano na Dr wa UNAMID kuhusu siku ya wanawake duniani

Mahojiano na Dr wa UNAMID kuhusu siku ya wanawake duniani

Wakati dunia leo ikiadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake na miaka 100 tangu kuanza kuadhimishwa siku hiyo, ofisi mbalimbali za Umoja wa Mataifa zinazoendesha operesheni katika nchi mbalimbali zimekuwa msitari wa mbele katika juhudi za ukombozi wa mwanamke.

Mpango wa Umoja wa Mataifa na ule wa Muungano wa Afrika kwenye jimbo la Darfur Sudan UNAMID nao hauko nyumba , una vitengo kadhaa vinavyoshughulikia masuala ya wanawake.

Moja ya vitengo hivyo ni kile cha ushauri wa masuala ya jinsia na mwandishi wa Umoja wa Mataifa Darfur Stella Vuzo amezungumza na Dr ambaye ni afisa wa kitengo hicho kuhusu siku ya wanawake na kazi zao za ukombozi wa mwanamke wa Darfur na Sudan kwa ujumla. Ungana nao

(MAHOJIANO NA DR JUDITH MAREMBE)