Skip to main content

Makubaliano ya Cancun yatekelezwe kwa vitendo:Figueres

Makubaliano ya Cancun yatekelezwe kwa vitendo:Figueres

Mkuu wa shirika la umoja wa mataifa linalohusika na hali ya hewa, ameyatolea mwito mataifa duniani kuharakisha utekelezaji kwa vitendo makubalino yaliyofikiwa kwenye mkutano wa Cancun na wakati huo huo ametaka mataifa hayo kuanisha njia mbadala itakayoanisha mustabala wa itifaki ya Kyoto inayohimiza mapinduzi ya kijani.

Christiana Figueres amesema kuwa mataifa duniani yanapaswa kuharakisha kuweka kwenye vitendo yale yaliyokubaliwa kwenye mkutano wa umoja wa mataifa mwaka uliopita katika mji mkuu wa Mexico Cancun. 

Ametaka shabaya kubwa sasa izingatiwe pia kwenye mkutano mwingine wa hali ya hewa unaofanyika mwaka huu huko Durban Afrika Kusin. Amesema kuwa makubaliano yaliyofikiwa huko Cancun ni hatua ambayo ulimwengu unapaswa kuyazingatia kwani yanatoa mwongozo wa namna ya kukabili changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa.