Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Libya inaendesha "mauwaji ya halaiki"

Libya inaendesha "mauwaji ya halaiki"

Serikali ya Libya imeshutumiwa kuwa inaendesha mauji ya halaiki na huku ikifanya matukio makubwa ya ufunjifu wa haki za binadamu ikiwemo kuwatesa raia wake na kuwaweka kizuizini.

Kulingana na Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay matumizi ya nguvu za kupindukia kama , helikopta, ndege za kijeshi na matanki makubwa ili kuwakandamiza waandamanaji knaweza kusababisha mauwaji ya maelfu ya watu.

 

Akihutubia kikao maalumu cha baraza la haki za binadamu Bi Pillay ametoa wito kwa jumuiya za kimataifa kuingilia kati ili umwagikaji wa damu zaidi nchini Libya.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)

 

Baraza hili  linakusudia kuunda jopo huru la uchunguzi kwa ajili ya kuangazia vitendo vya uvunjifu wa haki za binadam nchini Libya na kuwawajibisha wale wote watakaobainika kuhusika.