Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wengi waanza kuondoka Libya

Wahamiaji wengi waanza kuondoka Libya

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji, IOM watu hao ambao walikuwa wakifanya kazi katika maeneo mbalimbali wameondolewa baada ya serikali za Nepal, Philippines, Sri Lanka,Vietnam, Bangladesh, Moldova na Montenegro kuomba kuondolewa kwa raia wake.

Hata hivyo shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema kiasi cha dola za kimarekani millioni 11 zinahitajika ili kuwaondosha wafanyakazi wa kigeni 10,000 walioko nchini humo.

 

Akizungumzia hali jumla ya mambo nchini humo, msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Melissa Fleming amesema kuwa kundi jingine la wahamiaji haramu wapo mashakani na inawezekana wakashindwa kuondoka kutokana na kukosa utambuzi

 

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na chakula limesema kuwa Libya muagiza mkubwa wa chakula kutokana nje, lakini kutokana na mzozo huu unavyoendelea huenda ikakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa chakula.

 

Wakati huo huo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa huduma za usamaria mwema ili kuwasaidia kundi kubwa wa wakimbizi wanaomiminika katika nchi za Tunisia na Misri.

 

Ripoti za awali zinaonyesha kuwa jumla ya wahamiaji 22,000 wamerejea nyumbani Misri na Tunisia tangu kuzuka kwa machafuko hayo huko Libya