Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama wa wakimbizi wa Libya mashakani- UNHCR

Usalama wa wakimbizi wa Libya mashakani- UNHCR

Wakati maandamano yanayoenda sambamba na vitendo vya vurugu yakizidi kushika kasi nchini Libya, kuna wasiwasi kwamba hali ya usalama kwa wakimbizi nchini humo ni ya kiwango cha chini.

Duru zilizotolewa na Kamishna ya Umoja wa Mataifa juu ya wakimbizi zinasema kuwa wakimbizi wengi pamoja na wale wanaoomba hifadhi ya muda hawana uhakika juu ya usalama wao kutokana na kulengwa na makundi mbalimbali.

Afisa mmoja  anayehusika na wakimbizi anayefanya kazi na UNHCR Melissa Fleming amesema kuna uwezekano mkubwa wakimbizi hao wakaanza kukimbilia katika nchi za jirani na maeneo ya mbali kwa ajili ya kuomba hifadhi.

(SAUTI YA FLEMING)