Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM UM amtaka Qadhafi kukomesha matumizi ya nguvu dhidi ya waandamaji

KM UM amtaka Qadhafi kukomesha matumizi ya nguvu dhidi ya waandamaji

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mazungumzo kwa njia ya simu na kiongozi wa Libya Muammar al-Qadhafi ambaye anakabiliwa na shinikizo la kuachia madaraka toka kwa waandamanaji.

Ban ameelezea masikitiko yake kutokana na kuendelea kukua kwa matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji hao na akaitaka serikali ya Qadhafi isitishe mara moja mwenendo huo.

 

Amesema ni muhimu mamlaka za dola kutambua kwamba zinawajibika kuheshimu na kulinda uhuru wa maoni na haki za binadamu hivyo lazima matumizi ya nguvu yawekwe pembeni.

 

Akizungumza na waandishi wa habari hukoLos Angeles Ban ameonekana kukerwa na matukio ya utumiaji mabavu.

 

Wakati huo huo ofisi ya ubalozi wa Libya kwenye umoja wa mataifa imetangaza kuunga mkono maandamano hayo na kutaka umoja wa mataifa kuingilia kati.

Katika hatua nyingine Baraza la usalama linatazamiwa kukutana kujadilia hali hiyo ya Libya