Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikosi vya UM Sudan vyazidisha doria kwenye machafuko

Vikosi vya UM Sudan vyazidisha doria kwenye machafuko

Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Sudan vimeimarisha ngome ya ulinzi na wakati huo huo vimeanza kufanya doria kwenye maeneo ya Kaskazini na Kusin ambako hivi karibuni kuliripotiwa kuibuka kwa mapigano baina ya vikosi vya serikali na makundi ya waasi.

Kwenye mapigano hayo askari 54 walipoteza maisha na wengine 85 kujeruhiwa. Tayari Umoja wa Mataifa umetoa taarifa juu ya hali hiyo ikizitaka pande zote kujiepusha na machafuko yoyote.

Machafuko hayo ya hivi karibuni katika eneo lijulikanalo Malakal yalijitokeza siku moja tu kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya kura ya maoni juu ya Sudan Kusin ambayo imejitenga toka upande wa Kaskazin.